Maarif Islamiyya Education Website

Chuo Chetu

Historia Yetu

Chuo Kimesajiliwa kwa jina "THE REGISTERED TRUSTEES OF MAAHAD SHAMSIL MAARIF ISLAMIYA" Kwa No. 2072, Chuo kipo Mtaa wa Magomeni 'B', Kata ya Duga, Tarafa ya Pongwe, Jiji la Tanga - Tanzania.

Baada ya Kuasisiwa kilianza shughuli zake za ufundishaji katika msikiti ulio chuo hiki mtaa wa Majengo, Ilipofika mwaka 2001 kilipata eneo tajwa hapo juu lililokuwa na vyumba viwili tu hivyo tukaamua kufanya harambee ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambayo jiwe la msingi liliwekwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaji Ally Hasan Mwinyi.

Ilipofika mwaka 2002 tulipata mdhamini aliyetujengea jengo la ghorofa moja lenye vyumba vinne ambavyo vinatumika mpaka sasa.

Mikakati & Malengo

Malengo ya sasa ya chuo ni kuhakikisha kuboresha eneo la chuo katika upande wa majengo na kuhakikisha kunapatikana vyanzo madhubuti vya mapato yatakayosaidia kuhudumia walimu, wanafunzi na chuo kwa ujumla.

Chuo kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo;

  • Ukosefu wa bweni la wanafunzi
  • Vyumba vya Madarasa
  • Chakula cha Wanafunzi kwani wanafunzi wanaoishi chuoni wanajitegemea katika chakula
  • Mishahara ya Walimu kwani walimu wanaofundisha chuoni wamejitolea.

Malengo ya baadae ni kuhakikisha chuo kinakuwa na shule za chekechea, msingi, sekondari, kituo cha afya na kituo cha kulelea yatima.